Home Feedback Search

Mikopo; Kilimo na Mifugo
Home

Soma kipeperushi cha kuhusu mikopo ya pembejeo

       

United Republic of Tanzania, Ministry of Agriculture, Food Security & Corperatives, Agricultural Inputs Trust Fund. AGITF.  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, Mfuko wa Pembejeo.

Mikopo ya Pembejeo za Kilimo na Mifugo

 

Mfuko wa Pembejeo unatoa mikopo ifuatayo, mikopo ya pembejeo za kilimo na mifugo ambazo ni mbolea za aina mbalimbali za viwandani, mbegu bora, dawa za tiba na chanjo za mifugo, vyakula vya mifugo, dawa za kuhifadhi mazao ya kilimo na mifugo,  vifungashi vya mazao ya kilimo na mifugo na sumu za magugu, mikopo ya kununua  matrekta mapya, mikopo ya kuanzisha vituo vya kukodisha matrekta, mikopo ya kukarabati matrekta, mikopo ya kununua matrekta madogo ya mkono (Power tillers), mikopo ya zana ndogondogo za umwagiliaji,na zana ndogo ndogo za kilimo kama vile majembe ya kukokotwa na wanyama kazi (Plau).

 

1)   WALENGWA WA MIKOPO YA KUTOKA MFUKO WA PEMBEJEO

Walengwa wa mikopo ya pembejeo za kilimo na mifugo ni wakulima au wafugaji kupitia kwenye vikundi, wakulima au wafugaji binafsi, Vyama vya Msingi, Mifuko ya Pembejeo ya Wilaya, Vyama vya Kuweka na Kukopa (SACCOS) na mawakala wa kusambaza pembejeo wenye uzoefu usiopungua miaka miwili.

    

2)  UTEUZI WA WAOMBAJI WA MIKOPO
bullet
Halmashauri za Wilaya hutoa  tangazo la kuwapo mikopo kutoka Mfuko wa Pembejeo kama zilivyoainishwa hapo juu.
bullet
Waombaji  watatakiwa kujaza fomu maalum za maombi na kutoa maelezo binafsi, namba ya simu, anuani ya makazi na biashara/shamba ikiambatanishwa na mchanganuo wa matumizi ya mkopo anaoomba (Business plan), kivuli cha leseni hai ya biashara ya pembejeo kwa wafanya biashara na kivuli cha hati miliki ya dhamana ambacho mmiliki wake ndiye anayeomba mkopo.
bullet
Maafisa Kilimo/Mifugo wa Wilaya huthibitisha shughuli zinazoombewa mikopo katika wilaya husika kabla ya kuziptisha
bullet
Fomu za maombi zilizohakikiwa pamoja na vielelzo  vinavyohitajika hupitishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya/Miji/Manispaa/jiji.
bullet
Fomu za maombi na vielelezo vinavyohitajika pamoja na mahitaji ya pembejeo ya Wilaya husika hutumwa kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Pembejeo katika muda maalum kama ifuatavyo;

- Machi hadi Mei, mikoa ya Ruvuma, Rukwa, Mbeya, Iringa, Dodoma, Singida, Tabora, Shinyanga, Kigoma, Kagera, Mara na Mwanza.

- Agosti hadi Septemba, mikoa ya Arusha, Manyara, Kilimanjaro, Tanga, Morogoro, Pwani, Mtwara, Lindi na Dar es salaam.

bullet

Maombi haya huchambuliwa na kuwasilishwa kwenye kikao cha kamati ya mikopo na baadaye kwenye Bodi ya Wadhamini wa Mfuko ili yaidhinishwe.

bullet

Maamuzi ya Bodi  hutumwa kwa waombaji na kwenye Halmashauri za Wilaya husika.

 

3)      MASHARTI YA MIKOPO
  1.  Wakulima na wafugaji binafsi, kampuni na mawakala wa kuuza pembejeo, sharti wawe na dhamana isiyohamishika yenye hati miliki (Title deed) na inayokubalika kisheria. Mwombaji sharti awe ndiye mmiliki wa hati itakayodhamni mkopo. Mmiliki wa dhamana ya mkopo atatakiwa kupata uthibitisho kutoka ofisi ya ardhi iliko dhamana yake kuhusu uhalali wa umiliki wake na kwamba haina matatizo yoyote kwa kujaza consent letter.
  2. Kwa mikopo ya pembejeo mwombaji awe amefanya biashara ya pembejeo kwa muda usiopungua miaka miwili.
  3. Mifuko ya Pembejeo ya Wilaya isiyo na dhamana zenye hati miliki itadhaminiwa na Halmashauri za Wilaya husika.
  4. Vyama vya kuweka na kukopa (SACCOS), vikundi vya wakulima na wafugaji visivyo na dhamana za hati miliki sharti viwe viwe na akiba ambayo ni sawa na theluthi moja ya mkopo wanaoomba. Waombaji wa kundi hili watatakiwa kuwa wanachama wa asasi ya kifedha itakayotoa mkopo kwa niaba ya Mfuko wa Pembejeo.
  5. Mwombaji atatakiwa kulipia gharama za kutathmini dhamana ya mkopo wake  pamoja na asilimia moja (1%) ya mkopo utakaokuwa umeidhinishwa.
  6. Kwa mikopo ya matrekta mapya, mwombaji sharti awe na shamba binafsi lenye ukubwa usiopungua ekari 50 na awe tayari kutoa huduma ya kukodisha trekta hilo kwa wakulima wenzake.
  7. Mkopaji wa trekta  atatakiwa kulifanyia matengenezo madogo na makubwa trekta litakalonunuliwa kwa mkopo mara kwa mara kama atakavyoelekezwa na mtengenezaji au muuzaji wa trekta hilo. Aidha, trekta hilo litakuwa sehemu ya dhamana ya mikopo na kadi ya uandikishaji (Registration card) itakuwa chini ya umiliki wa Mfuko mpaka mkopo utakaporejeshwa.
  8. Muda wa kurejesha mikopo ya Mfuko wa Pembejeo ni  mwaka mmoja na nusu  kwa mikopo ya pembejeo za kilimo na mifugo, miaka miwili kwa mikopo ya kukarabati trekta, miaka mitatu kwa matrekta madogo ya mkono (power tiller) na miaka mitano kwa mikopo ya matrekta mapya.

 

 

 

Send mail to agitf@mari.or.tz with questions or comments about this web site.
Last modified: 03/06/07