Home Feedback Search

Mikopo Trekta Jipya
Home

Soma kipeperushi cha kuhusu mikopo ya pembejeo

       

United Republic of Tanzania, Ministry of Agriculture, Food Security & Corperatives, Agricultural Inputs Trust Fund. AGITF.  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, Mfuko wa Pembejeo.

Taratibu na Masharti ya Mikopo ya Kununua Trekta Jipya

1. Mwombaji atajaza fomu maalum ya maombi inayopatikana katika Ofisi za kilimo za Halmashauri za Wilaya na Makao makuu ya Mfuko wa Pembejeo, jijini Dar-es-salaam na katika tovuti yetu.

2. Fomu   za   maombi           zilizojazwa   na kuambatanishwa na vielelezo vinavyohitajika zitapitishwa/kuidhinishwa na Afisa Kilimo wa Maendeleo ya Mifugo wa Wilaya na Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya husika na baadaye kutumwa mapema kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Pembejeo.

3. 3. Mikopo ya kununua matrekta inatolewa na Mfuko wa Pembejeo, baadhi ya benki na taasisi za fedha na SCCULT (T) Ltd. kwa niaba ya Mfuko, mwombaji sharti atimize yafuatayo:-

  1. Awe na dhamana yenye hati miliki isiyohamishika iliyoandikishwa kwa jina la mwombaji.

  2. Awe na shamba binafsi lisilopungua hekta 50 na awe tayari kutoa huduma ya kuwalimia wakulima wengine

  3. Awe tayari kutekeleza masharti yote ya Mfuko wa Pembejeo au taasisi ya fedha na SCCULT yanayohusu mkopo wa ununuzi wa trekta jipya.

  4. Awe tayari kulipa asilimia moja (1%) ya mkopo kama gharama za nyaraka za mkopo na kusajili trekta kwa pamoja kwa jina lake na Mfuko

  5. Riba inayotozwa ni asilimia nane (8%) na marejesho hufanyika kwa muda wa miaka mitatu kila baada ya miezi mitatu.

 
 

 

Send mail to agitf@mari.or.tz with questions or comments about this web site.
Last modified: 03/06/07