Home Feedback Search

Mikopo na Walengwa
Home

Soma kipeperushi cha kuhusu mikopo ya pembejeo

       

United Republic of Tanzania, Ministry of Agriculture, Food Security & Corperatives, Agricultural Inputs Trust Fund. AGITF.  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, Mfuko wa Pembejeo.

Walengwa Wa Mikopo Ya Kutoka Mfuko Wa Pembejeo

Walengwa wa mikopo ya pembejeo za kilimo na mifugo ni wakulima au wafugaji kupitia kwenye vikundi, wakulima au wafugaji binafsi, Vyama vya Msingi, Mifuko ya Pembejeo ya Wilaya, Vyama vya Kuweka na Kukopa (SACCOS) na mawakala wa kusambaza pembejeo wenye uzoefu usiopungua miaka miwili.

 

Pembejeo zinazoweza kuombewa mikopo ni mbolea za aina mbalimbali za viwandani, mbegu bora, dawa za tiba na chanjo za mifugo, vyakula vya mifugo, dawa za kuhifadhi mazao ya kilimo na mifugo, sumu za magugu, vifungashi vya mazao ya kilimo na mifugo na zana ndogondogo za kilimo na mifugo za mikono au zinazokokotwa na wanyamakazi, kununua matrekta mapya na kukarabati matrekta mabovu.

 

Send mail to agitf@mari.or.tz with questions or comments about this web site.
Last modified: 03/06/07