Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Kilimo

WATAALAMU WAJENGEWA UWEZO WA UPIMAJI WA AFYA YA UDONGO

Imewekwa: 11 Oct, 2025
WATAALAMU WAJENGEWA UWEZO WA UPIMAJI WA AFYA YA UDONGO

Wataalamu mbalimbali kutoka Wizara ya Kilimo, Vyuo Vikuu pamoja na Taasisi zake  wamepatiwa mafunzo ya upimaji wa Afya ya Udongo tarehe 09 Oktoba, 2025 yaliyofanyika katika Chuo cha Mafunzo ya Kilimo cha MATI Ukirigulu kilichopo Mkoani Mwanza.

Mafunzo hayo chini ya uratibu wa Idara ya Usimamizi na Mipango ya Matumizi ya Ardhi za Kilimo yamelenga kuwajengea uwezo ili kuwa tayari kuanza zoezi la kupima afya ya udongo katika Mikoa ya Mwanza, Geita na Simiyu.

Mkurugenzi wa Mafunzo na Utafiti Wizara ya Kilimo, Dkt. Wilhelm Mafuru ambaye alimwakilisha Katibu Mkuu Gerald Mweli, amesema kuwa Serikali imepanga kutengeneza ramani ya kidigitali itakayotoa ikologia ya uzalishaji wa mazao nchi nzima.

Wataalamu hao wamepangwa kugawanyika katika Mikoa hiyo na Halmashauri zake ili kukusanya sampuli mbalimbali za aina ya udongo na kwenda kuzifanyia uchunguzi zaidi katika maabara.