Press Release
The Web Kilimo web
Home| Budget Speeches | Publications | Agricultural Statistics | Legislations and Regulations | Web Links

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA KILIMO CHAKULA NA USHIRIKA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI (PRESS RELEASE)

KUHUSU KUIDHINISHWA KUTUMIKA KWA
AINA MPYA ZA MBEGU ZA MAZAO

Kamati ya Taifa ya Mbegu (National Seed Committee) imeidhinisha matumizi ya aina 65 za mbegu mpya za mazao mbali mbali ya kilimo. Mazao hayo ni mahindi, mtama, ngano, muhogo, miwa, pamba, mbaazi, kunde, ufuta, korosho na tumbaku.  Hatua hiyo ya Kamati inalenga kuongeza tija na kipato kwa mkulima. 

Kuidhinishwa kwa aina hizo za mbegu kunafuatia mapendekezo yaliyofanywa na Kamati ya Taifa ya Kupitisha Aina Mpya za Mbegu za Mazao (The National Variety Release Committee) katika kikao chake kilichofanyika mjini Arusha tarehe 25 na 26 Februari, 2015.

Aina hizo mpya za mbegu zimepitishwa baada ya kufanyiwa utafiti na kugundulika kuwa zina sifa mbalimbali kama vile kutoa mavuno mengi, kustahimili ukame, ukinzani dhidi ya magonjwa, kukomaa mapema na kupendwa na wakulima.
Miongoni mwa aina hizo mpya za mbegu, kuna aina kumi na sita (16) za mahindi, mtama (2), ngano (3), muhogo (4), miwa (5), pamba (1), mbaazi (4), kunde (2), ufuta (1), korosho (24) na tumbaku (3). Mbegu hizo zimefanyiwa utafiti wa kina na vituo vya utafiti vya Umma na Sekta binafsi hapa nchini kama ifuatavyo:-

TAASISI/KAMPUNI

ZAO

AINA YA MBEGU

Kituo cha Utafiti Uyole

Mahindi

 • UHS 401

 

Ngano

 • Merina
 • Shangwe
 • Ngori

Kituo cha utafiti Ilonga

Pamba

 • NTA93-21

Mahindi

 • WE3117
 • WE3102
 • WE3113

Mbaazi

 • Kiboko
 • Ilonga 10-1M
 • Ilonga 10-2M
 • Karatu-1

Kunde

 • Vuli- 4

 

 • Vuli- 3

Kituo cha Utafiti Kibaha

Miwa

 • R570
 • R575
 • R579
 • N30
 • N41

Mihogo

 • Chereko
 • Kizimbani
 • Mkuranga-1
 • Kipusa

Kituo cha Utafiti Naliendele

Ufuta

 • Mtondo 2013

Korosho

 • Aina 24 kama zilivyoaainishwa katika jedwali lililoambatishwa

Meru agro tours & consultancyltd

Mahindi

 • MERU SB 507
 • MERU HB 509
 • MERU IR 621

SeedCo Tanzania company Ltd

Mahindi

 • SC 529
 • SC 533
 • SC 719

IFFA Seed Company Limited

Mahindi

 • Lubango Hybrid

Multi-Agro trading Main Supplier

Mahindi

 • MAMSH 591

Chareon Pokphand Produce Tanzania Co. Ltd

Mahindi

 • BSI 1
 • CP 808
 • CP 201

 

Advanta Seed Company

Mtama

 • PAC 501
 • PAC 537

East Africa Seed (T) ltd

Mahindi

 • KH 500-43A

Dandeva Seed Services (T) Ltd

Tumbaku

 • DDV 10
 • DDV 42
 • DDV 43

Sifa za aina hizo mpya za mbegu zilizoidhinishwa na Kamati ya Taifa ya Mbegu zimeainishwa katika Kiambatisho Na.1.

Aina hizo za mbegu zitaanza kuzalishwa na makampuni mbalimbali ya uzalishaji mbegu na Wakala wa Mbegu za Kilimo (Agricultural Seed Agency - ASA). Lengo ni kuzifikisha aina hizo za mbegu  bora kwa wakulima kuanzia msimu wa 2016/2017.

Imetolewa na:

 

Yamungu Kayandabila
KAIMU KATIBU MKUU


WIZARA YA KILIMO CHAKULA NA USHIRIKA

AINA MPYA ZA MBEGU ZA MAZAO ZILIZOIDHINISHWA NA
     KAMATI YA TAIFA YA MBEGU TAREHE 27 FEBRUARI, 2015

soma hapa

 

 

 

 

Previous Press Release

 
Speeches| Publications | Agricultural Statistics | Legislation and Regulations | About us|Contact us
Copyright 2008, Ministry of Agriculture Food Security and Cooperatives All rights reserved.