Press Release
The Web Kilimo web
Home| Budget Speeches | Publications | Agricultural Statistics | Legislations and Regulations | Web Links

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

 

 

 

WIZARA YA KILIMO CHAKULA NA USHIRIKA

 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU MKUTANO WA SHIRIKA LA SUKARI LA KIMATAIFA
MOUNT MERU HOTEL, ARUSHA TAREHE 31.05.2011 – 02.06.2011

Tanzania itakuwa mwenyeji wa mkutano wa 39 wa Shirika la Sukari la Kimataifa utakaofanyika katika hoteli ya Mount Meru, Arusha,  kuanzia tarehe 31 Mei mpaka tarehe 2 Juni 2011.

Mkutano utafunguliwa na Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Mhe. Profesa Jumanne Maghembe (MB) tarehe 31 Mei. Majadiliano yatalenga kwenye somo la “Fursa za Sekta ya Sukari katika Bara la Afrika”.

Mkutano huo pia unatoa nafasi ya kutangaza vivutio vya utalii vya pekee ambavyo vipo nchini.

Ufunguzi utafuatiwa na mada nane zitakazowasilishwa na watoa mada wa ndani na nje ya nchi, kuhusu masuala mbalimbali ya sekta ya sukari Tanzania, Afrika na Duniani. Siku ya pili Mkutano utajadili hali ya uchumi wa sukari duniani ikiwa ni pamoja na uzalishaji hali kadhalika masoko. Aidha, Kamati mbalimbali zitakuwa zinakutana kuandaa mkutano wa Baraza la Shirika la Sukari la Kimataifa utakaofanyika siku ya tatu.

Shirika la Sukari la Kimataifa (International Sugar Organisation) limeanzishwa chini ya Umoja wa Mataifa, wanachama wake wakiwa ni nchi mbalimbali. Kwa sasa, lina wanachama 86 ambao katika umoja huo wanachangia sehemu kubwa ya sukari inayozalishwa na inayotumika duniani.

Shirika linatoa nafasi nzuri kwa wadau wa sukari duniani kukutana na kujadili masuala ya uzalishaji na maendeleo ya uchumi wa sukari duniani. Kwa sasa wanachama wa Shirika la Sukari duniani ni wafuatao:- Argentina, Australia, Barbados, Belarus, Belize, Brazil, Cameroon, Chad, Columbia, Congo, Costa Rica, Cote d’Ivoire, Croatia, Cuba, Jamhuri ya Dominica, Ecuador, Misri, El Salvador, Ethiopia,  Austria, Belgium, Bulgaria, Cyprus, Jamhuri ya Czech, Denmark, Estonia, Finland, France, Germany,

Greece, Hungary, Ireland, Italia, Latvia, Lithuania, Luxembourg, Malta, Netherlands, Poland, Ureno, Romania, Slovakia, Slovenia, Hispania, Sweden, Uingereza, Fiji, Ghana, Guatemala, Guyana, Honduras, India, Indonesia, Jamhuri ya Kiislamu ya Watu wa Iran, Jamaica, Kenya, Jamhuri ya Watu wa Korea, Malawi, Mauritius, Mexico, Moldova, Morocco, Msumbiji, Nicaragua, Nigeria, Pakistan, Panama, Paraguay, Philippines, Shirikisho la Urusi, Serbia, Afrika  Kusini, Sudan, Swaziland, Switzerland, Tanzania, Thailand, Trinidad na Tobago, Tunisia, Turkey, Uganda, Ukraine, Umoja wa Falme za Kiarabu, Viet Nam, Zambia na Zimbabwe.

Mwaka huu 2011, Tanzania ndiyo Mwenyekiti wa Baraza la Kimataifa la Sukari. Nafasi hiyo inashikwa na Ndugu, Mohamed Muya, Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika. Hiyo ni heshima kubwa kwetu Tanzania,  hii ni mara ya kwanza kikao hiki kufanyika humu nchini. Hadi sasa, washiriki zaidi ya 80 kutoka nchi mbali mbali wamethibitisha kuhudhuria mkutano huo.

Tukiwa ndiyo wenyeji wa Mkutano huu, napenda kuchukua nafasi hii, kama Mwenyekiti wa Mkutano, kuwahimiza Watanzania wenzangu walio kwenye sekta ya umma na sekta binafsi, kutumia nafasi hii kuzungumza na wageni wetu miradi ya maendeleo, au biashara. Kama wapo watakaopenda ili wapangiwe nafasi ya kuonana na ujumbe kutoka nchi fulani, basi wawasiliane na waandaji  wa Mkutano ambao ni Bodi ya Sukari – Simu Na.2111523, Chama cha Wazalishaji wa Sukari (Tanzania Sugar Producers Association) Simu Na. 0713788285 na Mfuko wa Maendeleo ya Sukari Tanzania (Sugar Industry Development Trust Fund).

Mfuko huu ni chombo cha ushirikiano kati ya Serikali na sekta binafsi (public-private partnership) kilichoanzishwa hivi karibuni ili kusimamia masuala ya Utafiti, Mafunzo na Ugani, shughuli ambazo awali zilikuwa zinasimamiwa na Bodi ya Sukari. Mkutano wa wadau kama huu ni moja ya majukumu ya mfuko.

 

Imetolewa na:

 

Mohamed S. Muya
Mwenyekiti wa Mkutano na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika

Previous Press Release

 
Speeches| Publications | Agricultural Statistics | Legislation and Regulations | About us|Contact us
Copyright 2008, Ministry of Agriculture Food Security and Cooperatives All rights reserved.