MAANDALIZI YA SHAMBA LA BBT NDOGOWE
MAANDALIZI YA SHAMBA LA BBT NDOGOWE
Imewekwa: 04 Jan, 2025
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo anayeshughulikia Umwagiliaji na Ushirika, Dkt. Stephen Nindi ametembelea Shamba la Ndogowe lililopo chini ya programu ya Jenga Kesho iliyo Bora (BBT), mkoani Dodoma kukagua maendeleo ya shughuli mbalimbali zinazoendelea na utayari wa mapokezi wa vijana wa BBT.
Shamba hilo linatarajia kupokea Vijana 418 kwa awamu mbili za tarehe 12 na 13 Januari 2025 kwa ajili ya kuanza uzalishaji wa zao la mahindi na mazao mengine.
Dkt. Nindi ameongozana na Menejimenti ya Wizara pamoja na Mratibu wa programu ya BBT, Bi. Vumilia Zikankuba ambapo amepokea taarifa kuhusu maandalizi ya kupokea vijana, amekagua mabwawa ya maji ya umwagiliaji, nyumba za vijana watakazoishi, visima na miundombinu mingine ya shamba.