Dhamira na Dira
Dhamira na Dira
Dira
Kuwa kiini cha kutoa mwongozo wa sera na huduma kwa kilimo cha kisasa chenye tija, faida na ushindani kibiashara ili kuimarisha ustawi wa wananchi, usalama wa chakula na lishe ifikapo mwaka 2025.
Dhima
Kutoa huduma bora za kilimo, kuandaa mazingira bora kwa Wadau wa Kilimo, kuimarisha mfumo wa majadiliano ya Kisera, kuzijengea uwezo Mamlaka za Serikali za Mitaa na kuwezesha Sekta Binafsi kuchangia kikamilifu katika kilimo endelevu chenye tija, masoko ya uhakika na ongezeko la thamani ya mazao.
1.2.3 Malengo ya Wizara
Katika kufanikisha majukumu yake, Wizara inatekeleza Malengo Mkakati 10 kupitia Fungu 43, 24 na 05 katika Idara, Vitengo, Asasi, Mamlaka na Taasisi zilizo chini ya Wizara. Malengo Mkakati hayo ni: -
- Kuongeza tija na uzalishaji wa mazao ya Kilimo;
- Kuwezesha upatikanaji wa masoko ya mazao na bidhaa za Kilimo;
- Kuwezesha uongezaji wa thamani ya mazao ya Kilimo;
- Kuwezesha na kuimarisha Ushirika na Asasi za wananchi katika Kilimo na Sekta nyingine za kiuchumi;
- Kuimarisha mfumo wa ukusanyaji, uhifadhi, uchambuzi na usambazaji wa Takwimu;
- Kusimamia Sera, Sheria na Mikakati katika Sekta ya Kilimo;
- Kuboresha uratibu katika Sekta ya Kilimo;
- Kujenga, kuboresha na kusimamia miundombinu ya umwagiliaji
- Kuboresha uwezo wa Wizara wa kutoa huduma; na
- Kuzingatia masuala mtambuka katika Kilimo.