Muhtasari
Muhtasari
Malengo ya Wizara
Katika kufanikisha majukumu yake, Wizara inatekeleza Malengo Mkakati 10 kupitia Fungu 43, 24 na 05 katika Idara, Vitengo, Asasi, Mamlaka na Taasisi zilizo chini ya Wizara. Malengo Mkakati hayo ni: -
- Kuongeza tija na uzalishaji wa mazao ya Kilimo;
- Kuwezesha upatikanaji wa masoko ya mazao na bidhaa za Kilimo;
- Kuwezesha uongezaji wa thamani ya mazao ya Kilimo;
- Kuwezesha na kuimarisha Ushirika na Asasi za wananchi katika Kilimo na Sekta nyingine za kiuchumi;
- Kuimarisha mfumo wa ukusanyaji, uhifadhi, uchambuzi na usambazaji wa Takwimu;
- Kusimamia Sera, Sheria na Mikakati katika Sekta ya Kilimo;
- Kuboresha uratibu katika Sekta ya Kilimo;
- Kujenga, kuboresha na kusimamia miundombinu ya umwagiliaji
- Kuboresha uwezo wa Wizara wa kutoa huduma; na
- Kuzingatia masuala mtambuka katika Kilimo
Majukumu ya Wizara ya Kilimo:
Majukumu ya Wizara ya Kilimo yameainishwa katika Hati ya Mgawanyo wa Majukumu ya Mawaziri (Ministerial Instrument) ya tarehe 7 Mei, 2021. Majukumu hayo ni pamoja na: -
- Kuandaa na kutekeleza Sera za Kilimo, Usalama wa Chakula, Umwagiliaji na Ushirika;
- Kusimamia Matumizi Bora ya Ardhi ya Kilimo;
- Kufanya Utafiti, Mafunzo na Huduma za Ugani katika Kilimo;
- Kusimamia Usalama wa Chakula;
- Kusimamia Uhifadhi wa Kimkakati wa Chakula;
- Kusimamia Maendeleo ya Ushirika na Vyama vya Ushirika;
- Kuratibu Maendeleo ya Vyama vya Ushirika wa Akiba na Mikopo;
- Kuendeleza Miundombinu ya Kilimo;
- Kuratibu Masoko na kuongeza Thamani ya Mazao ya Kilimo;
- Kusimamia Maendeleo ya Zana za Kilimo na Pembejeo;
- Kuendeleza Kilimo cha Umwagiliaji;
- Kusimamia Maendeleo ya Rasilimali Watu Wizarani;
- Kusimamia leseni za stakabadhi za mazao ghalani; na
- Kusimamia Idara zinazojitegemea, Taasisi za Serikali, Wakala, Programu na Miradi ya maendeleo iliyo chini ya Wizara.