Mifumo ya Wizara
e-KILIMO
e-Kilimo ni mfumo wa kidijitali unaoratibiwa na Wizara ya Kilimo ili kuwezesha utoaji wa huduma bora kwa wakulima na wadau wa kilimo. Mfumo huu umejumuisha moduli mbalimbali zinazolenga maeneo tofauti ya huduma. Kupitia e-Kilimo, wakulima hupata huduma kwa haraka, taarifa sahihi na fursa za kuongeza tija.
Mfumo huu unapatikana kupitia:
- Tovuti: www.ekilimo.kilimo.go.tz na portal.kilimo.go.tz
- Programu ya simu janja: e-Kilimo kupitia Play Store
MFUMO WA CALL CENTRE
Call Centre ni mfumo unaomwezesha mkulima au mdau yeyote wa kilimo kupiga simu na kuuliza maswali kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na Wizara ya Kilimo. Kupitia mfumo huu, wananchi hupokea majibu ya papo kwa papo au mwongozo wa kitaalamu kutoka kwa maafisa husika. Mfumo huu unasimamiwa na Kitengo cha Mawasiliano cha Wizara ya Kilimo, na ni kiungo muhimu kati ya Serikali na wadau wa kilimo waliopo mashinani.
Mfumo huu unapatikana kupitia tovuti ya www.helpdesk.gov.go.tz
MFUMO WA HELPDESK
Mfumo wa Helpdesk ni jukwaa la kisasa linalowawezesha watumiaji wa mifumo yote ya TEHAMA chini ya Wizara ya Kilimo kuwasilisha changamoto wanazokutana nazo. Mfumo huu huratibu na kuhifadhi kumbukumbu za matatizo yote yaliyowasilishwa, namna yalivyopokelewa na hatua zilizochukuliwa hadi kutatuliwa. Kupitia mfumo huu: Kitengo cha TEHAMA hupata takwimu muhimu za kutathmini utendaji wa mifumo na maeneo yanayohitaji maboresho. Mfumo huu unapatikana kupitia tovuti ya
Mfumo huu unapatikana kupitia tovuti ya: www.helpdesk.gov.go.tz
MOBILE KILIMO
Online Systems - http://exts.kilimo.go.tz
Mobile Kilimo (M-Kilimo) ni teknolojia ya kutumia simu ambayo imelenga kuwasaidia wakulima, wafugaji na wavuvi kuyafikia masoko ya mazao yao kwa njia ya simu zao za mkononi. Hii itawafanya waweze kuyafikia masoko hasa hasa wanunuzi wa bidhaa na mazao yao ya kilimo pasipo…
AGRICULTURAL ROUTINE DATA SYSTEM〈ARDS〉
Online Systems - https://ards.kilimo.go.tz
Agricultural Routine Data System (ARDS) is a system whereby agricultural performance information are collected, managed and transmitted from LGAs to the ASLMs through Regions. The ARDS is composed of; 1) The VAEO/WAEO Format (Village/Ward Format),VAEO/WAEO 2) The Integrated…
Tanzania Agri-Inputs Platform