Naibu Katibu Mkuu anayeshughulia Mazao na Usalama wa Chakula, Dkt. Hussein Mohamed Omar amefanya ziara ya kikazi tarehe 20 Desemba 2024 kukagua shamba la majaribio ya tafiti za kilimo (TARI -Mkuranga) lenye ekari 2.6 na kujionea maendeleo ya uzalishaji wa miche ya nazi.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo anayeshughulikia Ushirika na Umwagiliaji, Dkt. Stephen Nindi, ameiagiza Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC) kuendelea kuimarisha na kuunda mifumo mbalimbali ya kidigitali ili kudhibiti upotevu katika Vyama vya Ushirika na kuwahakikishia wanaushirika usalama wa fedha zao hasa wanapofanya mauzo ya mazao yao.
Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe (Mb) akitoa maelekezo kwa Taasisi ya Kudhibiti Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI), Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) na Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) kukaa pamoja na kuunda jukwaa la wafanyabiashara wa pembejeo ambalo litakuwa na matawi matatu ya kusemea masuala ya mbolea, viuatilifu na mbegu.
Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe (Mb) akitoa maelekezo kwa Taasisi ya Kudhibiti Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI), Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) na Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) kukaa pamoja na kuunda jukwaa la wafanyabiashara wa pembejeo ambalo litakuwa na matawi matatu ya kusemea masuala ya mbolea, viuatilifu na mbegu.
Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe (Mb) amekutana na wadau wa Tasnia ya Mbegu na kujadili changamoto zinazoikabili tasnia hiyo, na kuwataka wazalishaji na wasambazaji wa mbegu kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuhamasisha wakulima kujisajili katika mfumo wa usajili wa ruzuku unaotumika kama njia ya mauziano ya pembejeo za kilimo nchini.
Waziri wa Kilimo, Mhe.Hussein Bashe (Mb) amekutana kwa mazungumzo tarehe 10 Desemba 2024 na wawakilishi kutoka Kampuni ya Nasa Corporation inayojishughulisha na utengenezaji wa mashine za kufungasha chai na wawakilishi kutoka Kampuni ya Kawasaki Kiko inayojishughulisha na utengenezaji wa mashine za kuchakata chai kutoka nchini Japan.
Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. David Silinde (Mb) akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC), Bw. Samuel Mshote wakati alipotembelea ghala la kuhifadhi mbolea lililopo eneo la Chuo cha Magereza, Ukonga, jijini Dar es Salaam tarehe 9 Desemba 2024.
Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. David Silinde (Mb) akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuthibiti Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI) Bw. Patrick Ngwediagi pamoja na watumishi wa Taasisi hiyo
Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. David Silinde (Mb) akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuthibiti Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI) Bw. Patrick Ngwediagi wakati alipotembelea ofisi za Taasisi hiyo iliyopo mkoa wa Morogoro
Kheri ya Miaka 63 ya Uhuru