Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Kilimo

Dkt. Mpango aweka jiwe la msingi katika kituo cha umahiri cha uhifadhi wa mazao ya nafaka, mtanana

06 Sep, 2024
12:00:00 - 15:00:00
Dodoma
HGCU

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango ameweka jiwe la msingi katika Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha Umahiri cha Uhifadhi wa Nafaka kilichopo Mtanana Wilaya ya Kongwa, mkoani Dodoma tarehe 20 Agosti 2024.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mhe. Dkt. Mpango amesema lengo la Serikali ni kuzidi kuboresha na kuinua uzalishaji wa mazao nchini ambapo ujenzi wa kituo hivho unatokana na Mradi wa  Kudhibiti Sumukuvu Tanzania (TANIPAC) ambao hadi sasa ujenzi wake umefika asimilia 96 ambapo utakapokamilika utagharimu Shilingi za Kitanzania 18,579,733,931.25.

“Lengo letu kama Serikali chini ya uongozi shupavu wa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kuboresha na kuinua uzalishaji katika Sekta ya Kilimo, ambapo kwa muda mrefu sehemu kubwa ya mazao yetu yamekuwa yakipotea. Tunataka kupunguza upotevu wa mazao baada ya kuvunwa,”amesisitiza Mhe. Dkt. Mpango.

Aidha, Dkt. Mpango ameeleza kuwa mradi wa kudhibiti sumukuvu utasaidia zaidi ya wakulima 12,517 waliopata mafunzo yaliyobora kuhusu Sekta ya Kilimo katika kupambana na sumukuvu kwenye mkoa wa Dodoma, hivyo Taifa limepata mwarobaini dhidi ya kuokoa maisha ya watu nchini.

Hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali akiwemo Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe (Mb); Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. David Silinde (Mb); Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Dkt. Hussein Mohamed Omar (Maendeleo ya Mazao na Usalama wa Chakula); Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo (Ushirika na Umwagiliaji), Dkt. Suleiman Serera; Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Bi. Rosemary Sinyamule; Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Bw. Job Ndugai pamoja na Waheshimiwa Wabunge

Dkt.  Mpango aweka jiwe la msingi katika kituo cha umahiri cha uhifadhi wa mazao ya nafaka, mtanana