Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Kilimo

VIJANA WA KUNDI LA KWANZA BBT WAMEWASILI WIZARA YA KILIMO KWA USAJILI KABLA YA KUELEKEA KWENYE SHAMBA LA PAMOJA NDOGOWE

Imewekwa: 12 Jan, 2025
VIJANA WA KUNDI LA KWANZA BBT WAMEWASILI WIZARA YA KILIMO KWA USAJILI KABLA YA KUELEKEA KWENYE SHAMBA LA PAMOJA NDOGOWE

Vijana wa kundi la kwanza la Programu ya Jenga Kesho iliyo  Bora (Build a Better Tomorrow- BBT) wamewasili na kuanza zoezi la usajili katika Wizara ya Kilimo kabla ya kuanza safari ya kuelekea kwenye shamba la pamoja la Ndogowe, mkoani Dodoma.

Vijana 103 wamepokelewa tarehe 12 Januari 2025 na kusajiliwa wakati awamu ya pili ya vijana wengine kuendelea kupokelewa tarehe 13 Januari 2025.  Shamba hilo la pamoja la Dkt. Samia Suluhu Hassan lililopo Mlazo /Ndogowe linatarajiwa kuwa na jumla ya vijana 418.