Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Kilimo

WAZIRI BASHE AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA MKUTANO WA CAADP

Imewekwa: 09 Jan, 2025
WAZIRI BASHE AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA MKUTANO WA CAADP

Mhe. Hussein Bashe (Mb), Waziri wa Kilimo ameongoza ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali za Umoja wa Afrika wa kupitisha Programu ya Kuendeleza Kilimo Barani Afrika (CAADP 2026 - 2035) unaofanyika nchini Uganda tarehe 9-11 Januari 2024.

Mawaziri wengine walioshiriki Mkutano huo ni Mhe. Jumaa H. Aweso (Mb.), Waziri wa Maji; Mhe. Shamata Shaame Khamis (Mb.), Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo - Zanzibar; na Mhe. Alexander P. Mnyeti (Mb.), Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi.

Mawaziri wa Sekta ya Kilimo watapitisha Mpango unaofuata wa Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo Barani Afrika ambao umejikita kwenye mifumo jumuishi ya uzalishaji wa chakula kwa kuzihusisha Sekta nyingine zinazochangia kwenye uzalishaji wa chakula ikiwemo miundombinu, elimu na afya.

Aidha, msimamo wa nchi kwenye kupitisha Mpango huo ni kuhimiza nchi wanachama kuichukulia Sekta ya Kilimo kwa mapana yake ili kuwa na uhuru wa chakula (food sovereignty) na kila nchi wanachama kuendelea kuwekeza kwenye Sekta ya Kilimo kwa upana wake pasipo kuathiri mazingira.