DKT. OMAR AMEIAGIZA CBT KUENDELEA KUHAMASISHA WAWEKEZAJI KUWEKEZA KATIKA KONGANI YA VIWANDA

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Dkt. Hussein Mohamed Omar (anayesimamia Usalama wa Chakula na Maendeleo ya Mazao) ameiagiza Bodi ya Korosho Tanzania (CBT) kuendelea kuhamasisha wawekezaji kuwekeza katika kongani ya viwanda inayojengwa kijiji cha Maranje Halmashauri ya Mji Nanyamba Wilaya ya Mtwara mkoani Mtwara
Akizingumza leo Februari 23, 2025 mkoani Mtwara alipotembelea kongani hiyo ya viwanda kwenye eneo hilo la Maranje, Dkt Omar amesema Serikali pekee haiwezi kuendelesha kongani hiyo hivyo wanahitaji uwekezaji kutoka sekta binafsi ambao wako tayari
‘’Lengo la Serikali ifikapo mwaka 2030 asilimia 100 ya korosho inayozalishwa yote ibanguliwe nchini, maana yake ni lazima tuwe na viwanda vya kutosha vya kubangua nchini na hii siyo pake yake na ufuta pia kwahiyo lazima tuwe na hivi viwanda vya kuongeza thamani,’’amesema Dkt. Omar.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa CBT, Mangile Malegesi amesema eneo lote hilo la kongani lina jumla ya hekari 1,572 linalotarajiwa kuwa viwanda zaidi ya 60 ambapo litagharimu takribani Sh bilioni 5.6 hadi kukamilika kwa mchakato huo mzima wa ujenzi.
‘’Kukamalika kwa maradi huu tunatarajia sasa kwa mkoa huu wa Mtwara na ukanda mzima wa kusini uchangamke zaidi kwani ajira zitakazopatiakana hapa hazitahusika tu watu wa mtwara bali hata kutoka nje ya mkoa na sehemu kubwa ni akina mama na vijana na ajira zitapatikana nyingi zaidi katika eneo letu hili la maranje,’’ amesema Bw. Mangile.
Kongani hiyo inakwenda kuongeza ajira 35 elfu za moja kwa moja, uuzaji wa korosho na bidhaa zake badala ya kuuza tu korosho ghafi kama vile ganda lenyewe.