DKT. OMAR ATOA RAI KWA WASINDIKAJI, WAZALISHAJI NA WASAMBAZAJI WA MBEGU ZA ALIZETI

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo anayesimamia Maendeleo ya Mazao na Usalama wa Chakula, Dkt. Hussein Mohamed Omar ametoa rai kwa wasindikaji, wazalishaji na wasambazaji wa mbegu za alizeti nchini kuingia mikataba na wakulima ili kuwawezesha kupata mahitaji mbalimbali ya kulima mbegu bora kwa ajili ya uhakika wa masoko.
Dkt. Omar ametoa rai hiyo wakati akifunga Kikao cha Wakulima na Wasindikaji wa zao la Alizeti tarehe 20 Machi 2025, Mkoani Singida.
Kikao hicho kililenga kuhimiza matumizi ya mbegu bora za alizeti ambapo Serikali kupita Wizara ya Kilimo inatoa ruzuku ya mbegu bora za zao hilo kwa bei ya shilingi 10,000 kwa kilo moja ukilinganisha na bei ya soko ya shilingi 45,000.
Kikao kilihudhuriwa na wakulima, wasindikaji, wazalishaji na wasambazaji wa mbegu za alizeti nchini.