Dkt. Serera azindua msimu wa kilimo 2024/2025 Mpwapwa, Pwaga
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo anayesimamia Ushirika na Umwagiliaji, Dkt. Suleiman Serera amezindua msimu wa kilimo wa 2024/2025 katika Wilaya ya Mpwapwa, kijiji cha Pwaga, Kata ya Pwaga tarehe 6 Desemba 2024.
Dkt. Serera amewapongeza wadau wa Wilaya Mpwapwa kwa kuweza kutekeleza mradi wa Stawisha Mpwapwa unaotekelezwa na Wilaya hiyo, huku akiwataka wakulima kuanzia sokoni na kumalizia shambani kwa kutambua mahitaji ya soko ili wanapojipanga kuingia shambani wazalishe kwa kuzingatia mahitaji ya soko.
Amesisitiza umuhimu wa kuendelea kutumia nguvu ya Ushirika ili kupata bei nzuri za mazao kupitia stakabadhi za ghala na minada. Aidha, amewasihi wadau kujitokeza kwa wingi ili kushirikiana na Serikali katika ujenzi wa miundombinu ya ghala za kuhifadhia mazao Wilayani humo.