MHE. SILINDE AMESHIRIKI KIKAO CHA BARAZA LA MAWAZIRI

Naibu waziri wa Kilimo, Mhe. David silinde (Mb), ameshiriki katika kikao cha Baraza la Mawaziri Kamisheni ya pamoja ya Bonde la mto Songwe tarehe 25 Februari 2025.
kikao hicho pia kimeudhuriwa na Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Eng. Kundo Mathew pamoja na wataalam mbalimbali wa Serikali kwa njia ya Mtandao jijini Dodoma.
Lengo la kikao hicho ni kujadili utekelezaji wa mradi wa kufua umeme katika Bonde la mto Songwe. Mradi huo utanufaisha wakulima wa kilimo cha umwagiliaji mkoani Songwe.
Baraza la Mawaziri wa Kamisheni ya Pamoja ya Bonde la Mto Songwe (The Joint Songwe River Basin Commission-SONGWECOM) ndiyo Chombo cha ngazi ya juu katika usimamizi wa Kamisheni hiyo. Baraza hilo linaundwa na Mawaziri kumi (10) kutoka katika sekta tano (5) za Maji, Nishati, Kilimo cha Umwagiliaji, TAMISEMI pamoja na Ardhi kutoka Tanzania na Malawi.