Mhe. Silinde: TOSCI hakikisheni Wafanyabiashara wa mbegu wanafuata utaratibu uliowekwa na Serikali
Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. David Silinde (Mb) ameitaka Taasisi ya Kuthibiti Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI) kuhakikisha wafanyabiashara wa mbegu za mahindi wanafuata utaratibu uliowekwa na Serikali ili kuongeza upatikanaji wa mbegu za mahindi zilizothibitishwa ubora ili kuongeza tija katika uzalishaji wa zao hilo.
Mhe. Silinde amesema hayo tarehe 7 Desemba 2024 wakati alipofanya ziara ya kikazi katika ofisi za TOSCI mkoani Morogoro ambapo alizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa TOSCI, Bw. Patrick Ngwediagi kuhusu Utekelezaji wa Mpango wa Ruzuku ya Mbegu za Mahindi kwa mwaka 2024/2025 pamoja na taarifa ya utekelezaji wa majukumu na mafanikio ya TOSCI.
Aidha, Naibu Waziri Silinde ameiagiza TOSCI kuhakikisha wafanyabiashara wanazingatia maelekezo ya Serikali ili kupunguza kudhibiti mauzo ya mbegu feki na changamoto nyingine zinazojitokeza kwenye Sekta ya Kilimo.