MKUTANO WA TATU WA G25 KAHAWA AFRIKA KULETA MAGEUZI TASNIA YA KAHAWA
MKUTANO WA TATU WA G25 KAHAWA AFRIKA KULETA MAGEUZI TASNIA YA KAHAWA
Imewekwa: 24 Feb, 2025

Mkutano wa Tatu wa G25 wa Kahawa Afrika umehitimishwa kwa kuweka wazi maazimio muhimu ya kuinua Tasnia ya Kahawa Barani Afrika.
Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameeleza kuwa kuna haja ya kuwa na mikakati ya kuinua zao la Kahawa ili kuepuka mabadiliko ya mara kwa mara ya bei katika soko la Dunia, hali inayowakatisha tamaa wakulima wengi.
Rais Samia amebainisha kuwa Afrika lazima iongeze jitihada katika kuboresha uzalishaji wa Kahawa na kuongeza thamani yake kupitia usindikaji wa ndani kwani ifikapo mwaka 2030, lengo ni kuona angalau asilimia 20 hadi 30 ya kahawa inayozalishwa Barani Afrika inasindikwa ndani ya Afrika badala ya kusafirishwa nje kama malighafi.
#3rdg25coffeesummittanzania