Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Kilimo

RAIS DKT. SAMIA ASHIRIKI MIJADALA INAYOHUSU KILIMO AFRIKA

Imewekwa: 11 Nov, 2024
RAIS DKT. SAMIA ASHIRIKI MIJADALA INAYOHUSU KILIMO AFRIKA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameshiriki katika mijadala muhimu ya kimataifa kuhusu kilimo barani Afrika ambayo ni  Africa Agriculture Dialogue (AAD) ulioandaliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB); na mjadala wa Kimataifa wa Norman E. Borlaug, ulioandaliwa na Taasisi ya World Food Foundation katika mji wa Des Moines, jimbo la Iowa, Marekani, mnamo Oktoba 30, 2024. Katika hotuba zake, Mhe. Rais Dkt. Samia ameeleza hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Tanzania ili kuwa mzalishaji mkubwa wa chakula kwa ajili ya kujitosheleza kama Taifa na kuuza Chakula cha ziada kibiashara (feed ourselves, feed others commercially).  Aidha, Mhe. Rais Dkt. Samia alibainisha jinsi nchi inavyoimarisha mifumo ya uzalishaji wa chakula kwa kutumia teknolojia za kisasa ili kufikia malengo hayo kama Taifa. Mikutano hiyo pia ilihudhuriwa na Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe (Mb); Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo wa Zanzibar, Mhe. Shamata Shaame Khamis (Mb); na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Bw. Gerald Mweli.