Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Kilimo

TARIBANI 4 na FHIA NI MKOMBOZI WA WAKULIMA WA NDIZI GAGERA

Imewekwa: 11 Nov, 2024
TARIBANI 4 na FHIA NI MKOMBOZI WA WAKULIMA WA NDIZI GAGERA
Ndizi aina ya TARIBANI 4 na FHIA zimetajwa kuwa ni mkombozi kwa wakulima wa mkoa wa Kagera katika kujihakiikishia usalama wa chakula pamoja na kipato. Akizungumza na wananchi waliofika kwenye banda la Taasisis ya Utafiti wa kilimo Tanzania (TARI) kwenye maonesho ya kuelekea siku ya chakula duniani yanayofanyika katika viwanja vya CCM Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera,  Meneja wa kituo cha TARI  Maruku, Dkt. Mpoki Shimwela amesema aina hizo za ndizi ambazo zimefanyiwa utafiti na TARI zinaa mikungu mikubwa na zinahilimili magonjwa ya migomba. “ Ndizi matoke aina ya Talibani 4 inahimili magonjwa na mgomba wake huzaa mkungu wenye uzito wa kati ya kilogramu 70 hadi 80 na FHIA inauwezo wa kuzaa mkungu wenye uzito wa kati ya kilogramu 50 hadi 100”. Amesema Dkt. Shimwela. Aidha Dkt. Shimwela ameongeza kuwa uwezo waw a migomba hiyo  kuzalisha mikungu mikubwa unaifanya TARI kupendekeza kwa wakulima kuzalisha zaidi aina hizo za ndizi kwani zinaweza kuinua Uchumi wa mkulima endapo atapanda kwa kufuata kanuni za kitalaamu. Dkt. Shimwela amekaribisha wananchi wote wa mkoa wa Kagera hususan wakulima kutembelea banda la TARI katika maonesho ya kuelekea siku ya Chakula Duniani katika viwanja vya CCM Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera.