Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Kilimo

WANANCHI KILOSA KUNUFAIKA NA SOKO LA MIWA

Imewekwa: 18 Feb, 2025
WANANCHI KILOSA KUNUFAIKA NA SOKO LA MIWA

Wananchi katika wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro wanatarajia kunufaika na soko la uhakika la zao la miwa kupitia kampuni hodhi ya Mkulazi inayomiliki kiwanda cha Sukari cha Mkulazi kikilenga kuongeza ukubwa wa mashamba ya wakulima toka
1,309 kufikia 1,717 za upandaji wa miwa kwa mwaka 2024/2025.
 
Mtendaji Mkuu wa Kampuni Hodhi ya Mkulazi, Bw. Selestine Some amesema wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge Viwanda, Biashara, Kilimo, Mifugo na Uvuvi tarehe 16 Februari 2025, mkoani humo.

Kiwanda hicho kina uwezo wa kuzalisha tani 50,000 kwa mwaka za sukari ya viwandani pamoja na majumbani, ambapo hadi sasa ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 98 na hadi kufikia Julai 2024/2025 jumla ya tani 19,124 za sukari zimezalishwa kati ya tani 20,000 ambazo zilipangwa kuzalishwa kwa msimu huu.

Kampuni hii pia inategemea miwa kutoka kwa wakulima waliojirani na kiwanda hicho ambapo kwa mwaka 2024/2025 kampuni ilinunua tani 37,981.89 za miwa toka kwa wakulima ikiwa ni zaidi ya lengo katika kununua tani 30,754 za miwa.

Katika kuongeza uzalishaji, kampuni ya shamba la miwa la Mkulazi imeendelea na programu ya kuwakopesha mbegu wakulima pamoja na huduma za kilimo ambapo kufikia Februari 2025, mbegu tani  6, 006.10 ziligawiwa kwa wakulima wa miwa mkoani humo.

Aidha, Kamati ilipongeza uendeshwaji wa kiwanda pamoja na chini ya kampuni hiyo, inayolenga kukabiliana na changamoto ya upatikanaji wa sukari ya viwandani ikitarajia kutoa ajira kwa watanzania 11,315 kwa mwaka 2025/26, Wajumbe wa Kamati hiyo pia walitembelea Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) Skimu ya Umwagiliaji ya Mkindo iliyopo wilayani Mvomero mkoani humo.