Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Kilimo

WANANNCHI WATAKIWA KUTUMIA FURSA YA MAONESHO YA SIKU YA CHAKULA DUNIANI

Imewekwa: 11 Nov, 2024
WANANNCHI WATAKIWA KUTUMIA FURSA YA MAONESHO YA SIKU YA CHAKULA DUNIANI
Wanachi wa Mkoa wa Kagera wametakiwa kushiriki kikamilifu katika maonesho ya siku ya chakula duniani yanayofanyika katika viwanja vya CCM manispaa ya Bukoba mkoani Kagera ili kuweza kujifunza mbunu mbalimbali za kilimo zinazotolewa na wataalamu katika mabanda ya maonesho. Hayo yamesemwa na wakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Muleba Mhe. Dkt. Abel Nyamahanga alipomuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Fatma Mwasa leo tarehe 13 Oktoba 2024  ambaye ni mgeni rasmi kwenye ufunguzi wamaonesho ya kuelekea kilelele cha siku ya chakula duniani ambayo kitaifa yanafanyika manispaa ya Bukoba mkoani Kagera. “Nimezunguka kwenye mabanda haya nimejifunza mengi hivyo kila mwananchi atafika kwenye viwanja hivi atapa elimu hii bure ambayo wataitumia katika maeneo yao ili kuendelea kuimarisha hali ya chakula”. Amesema  Dkt. Nyamahanga.   Mhe. Dkt. Nyamahanga amesema serikali inayoongozwa na  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan   imefanukiwa kuhajijisha uzalishaji wa chakula nchini unaimarika na kutosheleza mahitaji ya nchi nzima katika vipindi vyote. Awali Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Mazao wa Wizara ya Kilimo Bw. Nyasebwa Chimagu  aliyemuwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Bw. Gerald Mweli amesema Rais Samia Suluhu Hassan aliitangaza kwenye Mkutano wa Mifumo ya Chakula Afrika (AGRF) uliofanyika Mwezi Septemba 2023 kuwa Tanzania ipo tayari kuilisha  kwani itaweza kujilisha yenyewe na kuwalisha wengine kibiashara. Ameongeza kuwa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya juhudi kubwa kwenye maeneo ambayo yanaweza kufanikisha malengo hayo ikiwa  ni pamoja na  kuongeza tija na uzalishaji kwa kuwafikishia wakulima  mbolea,mbegu na viwatilifu. Bw. Chimagu amefafanua kuwa uzalishaji wa chakula katika kipindi cha uongozi wa  Dkt. Samia Suluhu Hassan umepiga hatua kutoka kutokomeza njaa na kuwa kilimo cha biashara  kwani uzalishaji umeongezeka kutoka tani milioni kumi na nne katika msimu wa mwaka juzi hadi tani tani milioni 22 kwa msimu uliopita.