Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Kilimo

Wazalishaji wa mbegu watakiwa kuimarisha miundombinu ya umwagiliaji

Imewekwa: 11 Nov, 2024
Wazalishaji wa mbegu watakiwa kuimarisha miundombinu ya umwagiliaji

Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. David Silinde (Mb) amewataka wazalishaji wa mbegu za kilimo kuimarisha miundombinu ya umwagiliaji katika mashamba ya kuzalisha mbegu ili kuwawezesha wakulima kupata mbegu kwa wakati. Mhe. Silinde ameyasema hayo tarehe 4 Oktoba 2024 wakati alipozindua rasmi  shughuli za uzalishaji wa mbegu za kampuni ya ACSEN Agriscience kutoka nchini India. Naibu Waziri Silinde ameongeza kuwa serikali itaendelea kufanya juhudi za kuhakikisha kuwa wazalishaji wa mbegu nchini wanapata masoko ya uhakia ndani na nje ya Tanzania.  Mhe. Silinde amefafanua kuwa Serikali kupitia Taasisi ya Uthibiti wa Ubora wa Mbegu za Kilimo Tanzania (TOSCI) imeendelea kuboresha maabara zake na shughuli za ukaguzi wa mashamba ya kuzalisha mbegu na kupelekea Tanzania kupata ithibati ya kimataifa hivyo basi wazalishaaji wa mbegu wana  fursa ya kuuza mbegu bora ndani na nje ya nchi. Mhe. Silinde amesisitiza kuwa Serikali itaendelea kuunga mkono juhudi za wawekezaji kwenye Sekta ya Kilimo kwa kuendelea kutoa ushirikiano kwa wawekezaji hao na endapo watakabiliana na changamoto wasisite kuwasiliana na Serikali ili zipatiwe ufumbuzi.  Awali Meneja wa kampuni ya ACDEN Agriscience Tanzania, Bw. Ravi  Periyasamy amesema kampuni hyo itazalisha mbegu bora zitakazohimili visumbufu na kuumpa mkulima mavuno yenye tija.