Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Kilimo

WAZIRI BASHE AMEKUTANA NA UONGOZI WA SHIRIKA LA MAENDELEO YA KILIMO (IFAD)

Imewekwa: 24 Jan, 2025
WAZIRI BASHE AMEKUTANA NA UONGOZI WA SHIRIKA LA MAENDELEO YA KILIMO (IFAD)

Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe (Mb) amekutana na Uongozi wa Shirika la Maendeleo ya Kilimo (IFAD) tarehe 22 Januari 2025 ofisini kwake jijini Dodoma na kufanya mazungumzo yaliyolenga kuendelea kudumisha ushirikiano katika kukuza Sekta ya Kilimo.

Ujumbe wa IFAD ulihusisha pia Bi. Sara Mbago-Bhunu, Mkurugenzi Mkuu wa Kikanda (Mashariki na Kusini mwa Afrika - IFAD), Bw. Sakphouseth Meng, Mkurugenzi Mkuu Mkazi na Mwakilishi wa Kanda (Mashariki na Kusini mwa Afrika - IFAD) pamoja na Bi. Jackline Machangu, Mratibu Mkuu wa IFAD nchini.