WAZIRI MKUU, MHE. MAJALIWA AZINDUA MRADI WA BBT PROJECT 1
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa (Mb) amezindua mradi wa BBT Project 1 inayofadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) tarehe 27 Aprili 2025, katika Viwanja vya Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Jakaya Kikwete, jijini Dodoma.
Uzinduzi huo umeshuhudiwa na Mhe. Hussein Bashe (Mb), Waziri wa Kilimo; Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi (Mb), Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo; Mhe. David Silinde (Mb), Naibu Waziri wa Kilimo; Bw. Gerald Mweli, Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo; Mhe. Rosemary Sitaki Senyamule, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma; Bw. Abdulmajid Nsekela, Mwenyekiti wa Kamisheni ya Tume ya Maendeleo ya Ushirika (TCDC); Dkt. Benson Ndiege, Mrajis na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC); Bw. Godfrey Ng’urah, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Ushirika Tanzania (CBT); Bw. Vianey Rweyendela, Mkurugenzi Mkazi wa AGRA; na Viongozi Wengine wa Serikali na Sekta Binafsi.
Mradi huu ni wa kwanza ikiwa ni mchango wa Washirika wa Maendeleo (Development Partners - DPs) ambapo utawezesha upatikanaji wa fedha kwa ajili ya kuendelea na utekelezaji wa Programu ya Vijana na Wanawake inayoitwa Jenga Kesho iliyo Bora (Build a Better Tomorrow -BBT).
Mradi huu utatekelezwa na Wizara ya Kilimo na Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia mwaka 2025 -2030; ambapo gharama ya mradi huo ni Dola za Marekani milioni 129.71.