Wizara ya Kilimo imepokea ujumbe kutoka DRC
Wizara ya Kilimo imepokea ujumbe kutoka DRC
Imewekwa: 05 Dec, 2024
Wizara ya Kilimo imepokea ujumbe kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) tarehe 4 Desemba 2024 jijini Dodoma uliohusisha wataalamu wanaotekeleza Programu ya Uendelezaji wa Masoko ya Mazao ya Kilimo inayoitwa AVENIR, chini ya ufadhili wa Shirika la IFAD.
Ujumbe huo unahusisha wataalamu kutoka Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, watendaji wa mradi wa AVENIR, wawakilishi wa wadau katika Sekta ya Kilimo nchini Kongo na Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania - MVIWATA.
Ujumbe huo ulipokelewa na Idara ya Masoko na Usalama wa Chakula iliyopo katika Wizara ya Kilimo ambapo lengo la ugeni huo ni kujifunza na kubadilishana uzoefu katika nyanja za masoko, usalama wa chakula na fursa za uwekezaji na masoko katika Sekta ya Kilimo.