Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Kilimo

ZIARA YA UKAGUZI WA JENGO LA KITEGA UCHUMI BODI YA TUMBAKU TABORA

Imewekwa: 19 Mar, 2025
ZIARA YA UKAGUZI WA JENGO LA KITEGA UCHUMI BODI YA TUMBAKU TABORA

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo, Mifugo na Uvuvi imefanya ziara Mkoani Tabora ya kukagua jengo la kitega uchumi la Ofisi ya Bodi ya Tumbaku tarehe 16 Machi 2025.

Mkurugenzi wa Bodi ya Tumbaku, Bw. Stanley Mnozya ameeleza kuwa jengo hilo lina thamani ya shilingi bilioni 1.2 ambapo litakuwa Makao Makuu ya Kanda ya Magharibi. Ujenzi huo umefikia asilimia 93 kumalizika ambapo kutakuwa na ofisi za bodi pamoja na ofisi kwa ajili ya kupangisha  taasisi zingine kama kitega uchumi.

Aidha, Mwenyekiti wa Kamati, Mhe. Deodatus Mwanyika (Mb) amepongeza ujenzi huo na kuelekeza kuwa marekebisho madogo madogo yaendelee hadi siku ya jengo kukabidhiwa na kuanza kutoa huduma. 

“Tunapongeza sana bodi kwa hatua hiyo ya mradi na nimefurahishwa sana kwa kuwapangisha Banki ya Ushirika ili wakulima wapate huduma hapa hapa badala ya kwenda Makao Makuu Dodoma.  Tumefurahishwa sana na hatua hii hivyo mkandarasi ajitahidi kukabidhi jengo kwa wakati,” amesema Mhe. Mwanyika.