Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Kilimo

Taarifa kwa Umma kuhusu maboresho ya Mfumo wa Vibali vya Kilimo (ATMIS)

15 Dec, 2024 Pakua

Wizara ya Kilimo inapenda Kuutaarifu Umma kuwa inatarajia kufanya maboresho ya mfumo wake wa kuombea Vibali mbalimbali vya Mazao na Viuatiliufu vya Kilimo kuanzia tarehe 14 Desemba 2024 saa sita(6) usiku hadi tarehe 15 Desemba 2024 saa sita(6) mchana. Hivyo kutakuwa na ukosefu wa huduma ya mfumo wa ATMIS kwa kipindi cha maboresho hayo.