Mhe. Hussein Bashe (Mb), Waziri wa Kilimo amefanya kikao kazi na Menejimenti ya Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC) inayoongozwa na Bw. Raymond Mndolwa, Mkurugenzi Mkuu pamoja na Wahandisi wa Umwagiliaji Mikoani tarehe 25 Machi 2025, jijini Dodoma.
Kikao hicho pia kimehudhuriwa na Dkt. Hussein Mohamed Omar, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo anayesimamia Maendeleo ya Mazao na Usalama wa Chakula.
Minister for Agriculture, Hon. Hussein Bashe (MP) met for a partnership discussion with the delegation from the African Development Bank Group (AfDB), led by Mr. Pascal Saginga on 26 March 2025, in Dodoma.
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali imeambatana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo anayesimamia Maendeleo ya Mazao na Usalama wa Chakula, Dkt. Hussein Mohamed Omar kutembelea ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji hekta 800 katika mashamba ya Wakala wa Mbegu za Kilimo (ASA)
Miundombinu ya Umwagiliaji katika shamba la Wakala wa Mbegu za Kilimo (ASA)
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo anayesimamia Maendeleo ya Mazao na Usalama wa Chakula, Dkt. Hussein Mohamed Omar akiwa na wasindikaji, wazalishaji na wasambazaji wa mbegu za alizeti nchini tarehe 20 Machi 2025, Mkoani Singida.
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Bw. Gerald Mweli amekutana na Viongozi wa Chama cha Wafanyabiashara wa Mbegu Tanzania (TASTA) na kujadiliana njia bora za utekelezaji wa ruzuku ya mbegu za mahindi kwa mwaka 2024/2025; ikiwa ni pamoja na mapendekezo mbalimbali ya uendelezaji wa tasnia ya mbegu nchini.
Kikao hicho kimefanyika tarehe 20 Machi 2025, katika ofisi za Wizara ya Kilimo jijini Dodoma na kuhudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu anayesimamia Ushirika na Umwagiliaji, Dkt. Stephen Nindi pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Mazao katika Wizara ya Kilimo, Bw. Enock Nyasebwa.
Wadau mbalimbali wa Sekta ya Kilimo wanaotekeleza Programu ya Mifumo Himilivu ya Chakula Tanzania (TFSRP) tarehe 17 na 18 Machi, 2025 wameshiriki mafunzo elekezi ya kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa (Climate Adaption) yaliyotolewa na Benki ya Dunia (WB) kwa kushirikiana na Global Climate Adaption (GCA) katika Ukumbi wa Nashera jijini Dodoma.
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) ikikagua ujenzi wa mradi wa vihenge na maghala ya kisasa vya kuhifadhia mazao vinavyosimamiwa na Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA), wilaya ya Babati, Mkoa wa Manyara
Mradi wa vihenge na maghala ya kisasa kwa ajili ya kuongeza uwezo wa kuhifadhi nafaka unaosimamiwa na Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA)